Serikali ya Kenya imepiga marufuku maandamano ya aina yoyote nchini humo, kufuatia vifo vya watu kadhaa, baada ya ghasia kukumba taifa hilo la Afrika Mashariki, yaliyoandaliwa na muungano wa upinzani CORD.
Hayo yamesemwa hivi punde na waziri wa usalama wa ndani nchini humo, Bwana Joseph Nkaissery, katika kikao na wanahabari.