Home » 2016 » June » 11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri huku akimteua Mbunge wa Buchosha Dk. Charles Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Category: HABARI | Views: 325 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)



Ifuatayo ni miji 16 yenye mifumo ya usafiri ambayo ni hatari zaidi kwa wanawake. 
Category: HABARI | Views: 290 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)



Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Shuaibu Amod amefariki ucku wa kuamkia leo. Kocha huyo ambaye inasemekana jana siku ya ijumaa alikuwa akisema kuwa kifua kina muuma na hivyo kuamua kwenda kulala. Kifo chake kimegunduliwa baada ya kocha huyo kushindwa kuamka tangu alipokuwa amelala usiku wa jana. Kocha huyo amefariki akiwa na miaka 58.
Category: MICHEZO | Views: 340 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)

Staa wa Bongo Fleva ambaye pia ni mwalimu wa dance, Msami Giovanileo June 11, 2016 anazimiliki headlines za kufanyiwa suprise ya nguvu na uongozi wake baada ya kupewa zawadi ya gari mpya.

Ni gari aina ya Toyota Ipsum ambayo imenunuliwa kwa kiasi cha shilingi milioni 15 baada ya single yake iitwayo Mabawa kufanya vizuri katika vituo mbalimbali.
Category: BURUDANI | Views: 360 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)



Klabu ya Simba, imefanikiwa kuinasa saini ya winga mwenye kasi wa Mwadui FC, Jamali Mnyate aliyesaini mkataba wa miaka miwili kwa ada ya Tsh. Milioni 15.

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia Goal, tayari wamemaliza zana na mchezaji huyo na sasa ni mali yao.
Category: MICHEZO | Views: 355 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)



Watu sita wamefariki Dunia na wengine nane wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Hiace lililokuwa likitokea Mjini Same likielekea Njoro Wilayani Same, ambapo liligongana na gari ya mizigo aina ya Fuso muda mfupi baada ya kuondoka katika Kituo cha abiria cha Same Mjini.
Category: HABARI | Views: 316 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)

MLALAMIKIWA wa kwanza katika kesi ya uchaguzi Jimbo la Longido mkoa wa Arusha, Mbunge wa Longido, Onesmo ole Nangole (Chadema), ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuwa anajua kusoma na kuandika Kiswahili, lakini hajui kusoma na kuandika Kiingereza.
Category: HABARI | Views: 324 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)

Mchezaji, mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amethibitisha kwamba ni moto wa kuotea mbali baada ya kuweza kufunga magoli 3 katika mechi ambayo aliingia kipindi cha pili na kuisaidia timu yake ya taifa kushinda magoli 5-0 dhidi ya taifa la panama. 
Category: MAGAZETI | Views: 285 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)



Walipakodi wote wanakumbushwa kuzingatia mwisho wa kulipa kodi ya Mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) PASIPO ADHABU
1.O    ULIPAJI WA KODI YA MAPATO – MAKADIRIO YA AWALI
⦁    walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/06/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya nne ya makadirio ya awali ya mwaka 2016
⦁    walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/09/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya tatu ya makadirio ya awali ya mwaka 2016
⦁    walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/12/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya pili
⦁    walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 31/03/2017, wanapaswa kulipa sehemu ya kwanza ya makadirio ya awali ya mwaka 2017
 
Category: HABARI | Views: 297 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)

Hii ni orodha ya nchi ambazo raia wa mataifa ya ulaya wanaamini ndizo zenye maisha bora zaidi. Orodha hii inaonyesha kila raia wa taifa fulani na nchi wanayoamini ni bora. Katika orodha hii Ugiriki ndiyo taifa ambalo linaaminiwa kuwa na maisha ovyo kabisa kwa ulaya. 
Category: HABARI | Views: 294 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)


Tamisemi Yakanusha Taarifa Kwenye Mitandao Ya Jamii Juu Ya Kusitisha Ajira Za Walimu Wapya 2015/2016
Category: HABARI | Views: 335 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)

Category: MAGAZETI | Views: 342 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)


Kijana mmoja nchini  Marekani aitwae Stan Larkin ameweza kuishi siku 555 bila kuwa na moyo kufuatia moyo wake kuondolewa kabisa kutoka kwenye mwili wake. Baada ya kuondolewa moyo kifaa maalum aliwekewa na wataalamu cha kumsaidia kufanya kazi huku akisubiri huduma ya kubadilishiwa moyo(transplanting) 
Category: HABARI | Views: 300 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)




Ufaransa imefanikiwa kuanza vizuri michuano ya Euro 2016 ikiwa mwenyeji baada ya kuifunga timu ngumu ya Romania kwa mabao 2-1.
Huo ndiyo ulikuwa mchezo wa kwanza au wa ufunguzi wa michuano hiyo itakayochezwa nchini Ufaransa.
 
Category: MICHEZO | Views: 308 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)