Home » 2016 » June » 13


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo leo.
Category: HABARI | Views: 316 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-13 | Comments (0)

Eritrea imeishtumu Ethiopia kwa kutekeleza shambulio katika mpaka wake ambao una ulinzi mkali.

Wakazi katika eneo la Tsorona wanasema wamesikia milio ya risasi na kuona wanajeshi wakielekea katika mpaka.

Hata hivyo Waziri wa habari wa Ethiopia amesema hafahamu lolote kuhusu vita hivyo.

Zaidi ya watu laki moja walifariki katika mapigano yaliyodumu mika miwili na nusu katika ya mataifa yote mawili.

Category: HABARI | Views: 306 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-13 | Comments (0)

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri.

Jumamosi iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.

Category: HABARI | Views: 292 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-13 | Comments (0)

Marafiki wawili na wafanyabiashara nchini Uganda Mr Steven Wesonga na Mr David Woisi wamekubaliana wikend iliyopita juni 11 mbele ya wanakijiji kubadilishana wake zao.Mr Wesonga akamchukua Ms Sara Mdua ambaye ni mke wa Woisi na Mr Woisi akamchukua Ms Annette Namataka ambaye ni mke wa Wesonga.Bwana Wesonga amezaa watoto watano na mke wake huyo wa zamani wakati Woisi amezaa watoto wawili na mke wake huyo wa zamani.

Category: HABARI | Views: 313 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-13 | Comments (0)