Wachezaji wa klabu ya soka ya Enyimba nchini Nigeria wamelalamikia uongozi wa klabu hiyo kutowalipa mishahara yao kwa muda wa miezi mitatu. Mmoja ya wachezaji wa klabu hiyo hiyo ambaye alionyeshwa kuchukizwa na kitendo hicho amewaambia waandishi wa habari kuw
Chama cha soka barani Ulaya kimefuta kesi iliyokuwa inamkabili mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho baada ya kusikiliza kesi hiyo. Katika kusikilizwa kesi hiyo pia walihudhuria wakili wa mchezaji huyo pamoja na mjumbe maalumu anayehusika na kitengo cha kusimamia matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Rooney ambaye alijikuta matatani muda wa mwisho wa kocha alistaafu klabuni hapo Alex Ferguson baada ya kuhamishwa kutoka nafasi aliyozoea ya kucheza kama mshambuliaji na kurudishwa nyuma kama kiungo.
WAUMINI zaidi ya 300 kutoka mikoa mbalimbali nchini waliokuwa wameweka kambi kwa ajili ya kushiriki kongamano la Kanisa la Sauti ya Uponyaji la Nabii Joshua, eneo la Kihonda- Veta, Manispaa ya Morogoro wamelazimika kurejea makwao kutokana na kongamano hilo kusitishwa, baada ya baadhi yao kuugua ugonjwa wa kipindupundu na kulazwa kambi maalumu ya Kituo cha Afya cha Sabasaba cha mjini Morogoro.
HUZUNI imetanda katika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, baada ya ajali ya moto wa kibatari kuteketeza watoto wanne wa mama mmoja, waliokuwa wamefungiwa chumbani na dada anayewalea.
Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Lwema ametishia kumburuza mahakamani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Godfrey Sanga kwa madai ya kuendelea kutoza ushuru wa mazao baada ya kufutwa na Serikali mwaka 2002.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe ameridhia kufutwa kwa bodi za wadhamini na taasisi mbalimbali zisizokuwa za kiserikali 680 ambazo haziko kisheria. Pamoja na hayo kairuhusu Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuzisajili upya wadhamini wa asasi, na taasisi mbalimbali.
Kituo cha televisheni cha Clouds kimetakiwa kuomba radhi kwa siku tano kupitia taarifa zake za habari kutokana na maudhui ya kipindi cha Take One kilichomuonyesha mwanaume anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja.