Home » 2016 » August » 07
Makumi ya Wamarekani wameandamana katika mji wa Chicago nchini Marekani wakipinga ubaguzi wa rangi na vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji yanayofanywa na polisi wa nchi hiyo dhidi ya Wamarekani weusi.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamepiga nara za kulaani mauaji ya polisi ya hivi karibuni nchini humo dhidi ya kijana mmoja mdogo mwenye asili ya Afrika. 
Category: HABARI | Views: 439 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)

Ripoti ya siri iliyotolewa hivi karibuni kuhusiana na shambulio a kigaidi ya Septemba 11 nchini Marekani mwaka 2001 inaonesha kuwa, Bandar bin Sultan Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi na Saudia na balozi wa wakati huo wa Saudia mjini Washington alikuwa na uhusiano na mmoja wa wafuasi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda aliyetekeleza shambulio hilo la kigaidi
Category: HABARI | Views: 331 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)


Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 tulieleza malengo yetu kwa wananchi. Tunawakumbusha malengo hayo. Tutakuwa tunatoa mrejesho wa utekelezaji kila wakati. Siku ya Jumanne tarehe 9/8/2016 tutatoa mrejesho wa kwanza.
Category: HABARI | Views: 285 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)

Duru za kuaminika zimeripoti kuwa watu saba wameuawa nchini Ethiopia katika maandamano ya kupinga serikali.
Kwa mujibu wa duru hizo watu wasiopungua saba wameuawa katika makabiliano yaliyotokea kati ya askari polisi na waandamanaji katika mji wa Nemekte Wollega magharibi mwa nchi hiyo. Duru hizo zimeongeza kuwa kwa miezi kadhaa sasa watu wa makabila mawili ya Oromo na Amhara wamekuwa wakimiminika mabarabarani kuandamana wakilalamikia siasa za serikali ya Addis Ababa.
Category: HABARI | Views: 308 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)



Katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa Afrika Kusini, chama tawala cha ANC, kimeshindwa na Democratic Alliance, katika eneo lenye mji mkuu,Pretoria.
Category: HABARI | Views: 296 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameuagiza uongozi wa Jeshi la Magereza mkoani Iringa kuanza mchakato wa kulhamisha gereza kuu la mkoa huo kutoka katikati ya mji na kwenda pembezoni mwa mji.
Category: HABARI | Views: 280 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)

Chadema imetangaza kufanya mikutano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi katika operesheni iliyobatizwa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), ikidai Serikali ya Awamu ya Tano inakandamiza haki na demokrasia nchini.
Category: HABARI | Views: 324 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)

 
 
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni amesema askari wa usalama barabarani watakaobainika kupokea rushwa watashughulikiwa kwa kuwa wataweka mitego kwa ajili ya kuwakamata.
Category: HABARI | Views: 267 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)

 
 
MWANAFUNZI aliyekuwa akisoma Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Zimba, Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Susana Kauzeni (15) ameuawa baada ya kupigwa na wazazi wake wakimtuhumu kuwa ni mtoro sugu wa shule.
Category: HABARI | Views: 287 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)



Kutoka nchini Hispania kwenye klabu ya Real Madrid imeripotiwa kuwa kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane na raisi wa klabu hiyo Florentino Perez wapo kwenye malumbano makubwa ya kiungo gani anatakiwa kusajiliwa na klabu hiyo. 
Category: MICHEZO | Views: 314 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)



Mchezaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa Ufaransa Paul Pogba huenda akafanyiwa vipimo vya afya leo kwenye klabu ya Manchester united ili kukamilisha uhamisho wake. 
Category: MICHEZO | Views: 372 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)

 
 
SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.
Category: HABARI | Views: 291 | Added by: nurdidy | Date: 2016-08-07 | Comments (0)