Home » 2016 » June » 07
Polisi mkoani hapa wametumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya wananchi wanaokutwa wamekusanyika katika maeneo mbalimbali.

Category: HABARI | Views: 294 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-07 | Comments (0)




Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya Mikopowww.heslb.go.tz
IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016
 
Category: HABARI | Views: 297 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-07 | Comments (0)



Siku chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo  kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.
Category: HABARI | Views: 299 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-07 | Comments (0)

Category: MAGAZETI | Views: 356 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-07 | Comments (0)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila alitoa agizo hilo jana kupitia taaarifa kwa vyombo vya habari. 
 
Profesa Msanjila alisema hatua hiyo, inatokana na kubainika kwamba wanafunzi hao hawastahili kusoma shahada na pia hawakustahili kupewa mkopo.
Category: HABARI | Views: 312 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-07 | Comments (0)

RAILA Na LEONARD ONYANGO KIONGOZI wa Cord, Raila Odinga, alidai jana kuwa makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) sasa wameanza kutuma wajumbe wakitaka azungumze nao.

Akihutubia mamia ya wafuasi wa muungano huo katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi, baada ya maandamano ya amani katikati mwa jiji, Bw Odinga alidai alitumiwa mjumbe na IEBC kumsihi wazungumze kumaliza mzozo.

 

Category: HABARI | Views: 304 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-07 | Comments (0)

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, msemo huo ndiyo unaweza kutumika kuelezea tukio la Daniel Mshana (41), mkazi wa Njiapanda ya Himo wilayani Moshi, ambaye ameamua kumbaka binti yake wa kumzaa.

Kitendo hicho kiligunduliwa na walimu wa shule aliyokuwa akisoma mtoto huyo mwenye umri wa miaka tisa, baada kuona nuru ya uchangamfu ikififia na kiwango chake cha kufaulu kikianza kuporomoka.

Category: HABARI | Views: 340 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-07 | Comments (0)