Home »
2016 » June » 07 » RAILA-IEBC WANATAKA TUONGEE
2:20 AM RAILA-IEBC WANATAKA TUONGEE |
\\
“Ati jana (Jumapili) maafisa wa IEBC walinitumia mtu wakitaka nifanye mazungumzo nao. Sisi kama Cord tunasema kwamba wakati wa mazungumzo na IEBC umepita kwani tulijaribu kufanya nao mazungumzo wakatukwepa,” akasema. Huku akiuliza wafuasi wa Cord iwapo wanataka aongee na maafisa wa tume hiyo, Bw Odinga alisema wakati wa kuongea na IEBC umeshapita.
“Tuliwapa nafasi wakaipoteza. Tunachotaka kuzungumzia ni hatua tutakazochukua baada ya makamishna wa tume hiyo kuondoka,” akasema.
Kinara mwenza wa Cord, ambaye ni Seneta wa Bungoma, Moses Wetang’ula, alirudia madai hayo akisema makamishna wa IEBC walijaribu kumshawishi Bw Odinga afanye mazungumzo nao.
“Jana (juzi) ndugu yangu Raila alinipigia simu akaniambia kwamba IEBC wanataka kuzungumza nasi. Lakini sisi tunasema hatuwezi kuketi chini na makamishna hao. Tunataka waondoke,” akasema.
Hata hivyo, afisa wa uhusiano mwema wa IEBC, Bw Andrew Limo, alikanusha madai hayo akisema hakuna afisa yeyote wa IEBC aliyeenda kwa Bw Odinga kutaka mazungumzo.
|
|
Category: HABARI |
Views: 305 |
Added by: nurdidy
| Rating: 0.0/0 |