Aidha amesema bodi ya mikopo nchini imetumia makampuni ya udalali kukusanya madeni kwa wanafunzi kwa makubaliano ya malipo ya Asilimia 2.5 ya deni la mdaiwa, ambayo makampuni mengine hayajasajiliwa na mengine yamesajiliwa kuuza vifaa vya ujenzi wakati wadaiwa wanawadhamini na kusababisha watu kubambikiwa madeni ili madalali wapate kamisheni kubwa.
Category: HABARI |
Views: 298 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
Siku ya jana jumanne tarehe 14/06/2016 mchezaji kutoka nchini Cameroon Samuel Etoo amefunga ndoa na mpenzi wake wa tangu muda mrefu Georgette Tra Lou katiiliyofanyika zuri iliyofanyika nchini Itali. Katika sherehe hiyo walihudhuria watu wengi maarufu akiwemo aliyekuwa beki wa Barcelona Carlos Puyol.
Category: MICHEZO |
Views: 346 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
 Zaidi ya tani 1,150 za sukari zinatarajia kuingia mkoani Mbeya kuanzia leo kutoka nchini Malawi kwa lengo la kupunguza uhaba wa bidhaa hiyo. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa mkoani hapa katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini, kwa lengo la kusikiliza kero zao.
Views: 296 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
 Ratiba ya msimu mzima ya klabu ya Arsenal ligi kuu Uingereza 2016/2017 hii hapa.
Category: MICHEZO |
Views: 286 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
Ratiba ya mechi za ufunguzi za ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2016/2017 hii hapa.
Category: MICHEZO |
Views: 267 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
Mmiliki mpya wa klabu ya Aston villa ya nchini Uingereza na bilionea kutoka nchini ChinaTony Xia wamefanya mkutano wao wa kwanza na waandishi wa habari wakiwa pia na kocha mpya wa klabu hiyo De Matteo huku akisema amenuia kuifanya klabu hiyo kuwa kubwa na ya ushindani kama zilivyo Real Madrid na Barcelona.
Category: MICHEZO |
Views: 264 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
 Rais wa Marekani, Barack Obama, ameshtumu vikali matamshi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwamba waislamu wasiruhusiwe kuingia Marekani. Obama amesema hiyo 'si marekani wanayohitaji.'
Category: HABARI |
Views: 286 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
 Jaji nchini Uganda ametoa amri kuwa kesi ya kiongozi wa upinzani nchini humo Kizza Besigye, ifanyike mahakamani kwa makosa ya uhaini na wala sio kwenye gereza lenye ulinzi mkali ambapo anazuiliwa.
Category: HABARI |
Views: 272 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
Roboti kwa jina Pepper, iliyotengenezwa kuelewa hisia za watu inatarajiwa kuanza kazi mpya kama karani wa mapokezi katika hospitali mbili nchini Ubelgiji.
Roboti hiyo itakuwa ya kwanza kuhudumu katika jumba la matibabu baada ya roboti nyengine kuwekwa katika maduka ya uuzaji bidhaa, benki na vituo vya treni.
Hospitali moja inamipango ya kuajiri roboti zaidi kwa miaka 10 ijayo.
Baadhi ya wataalamu wamehoji umuhimu wa roboti za kijamii kama vile Pepper.
Category: HABARI |
Views: 292 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
WAKATI kesho Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikitarajiwa kutimiza azma yake ya kuzima simu ‘feki’ za mkononi, upo mtikisiko na kizaazaa miongoni mwa watumiaji wa vifaa hivyo vya mawasiliano, wakisaka mbadala na wengine wakisubiri kuona kama ‘yatatimia’.
Category: HABARI |
Views: 298 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
MWANASIASA mkongwe nchini na Naibu Waziri Mkuu mstaafu, Agustine Mrema amewataka wapinzani kumwacha Rais Dk. John Magufuli afanye kazi yake kwa kuwa amechaguliwa kihalali na bado hajamaliza hata kipindi cha kwanza cha uongozi wake.
Amewatahadharisha wananchi kuwa makini na wanasiasa kwa kuwa wapo baadhi wasio na nia njema na nchi badala yake wamekuwa wakipigania maslahi yao binafsi hata kama nchi inaweza kuingia kwenye majanga.
Category: HABARI |
Views: 291 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
Chadema imeondoa mahakamani kesi dhidi ya polisi ya kupinga amri ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara, baada ya kubainika mapungufu ya kisheria katika hati yao ya mashtaka.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake jana, Jaji Mohamed Gwae aliyepangwa kusikiliza shauri hilo alitaja mapungufu ya kisheria yaliyobainika kwenye hati ya mashtaka ya Chadema kuwa ni pamoja na kumjumuisha katika hati ya mashtaka Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya, ambaye kisheria alistahili kufunguliwa shtaka katika masjala kuu (main registry).
Category: HABARI |
Views: 267 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-15
|
|
|