Home » 2016 » June » 27

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na kampuni ya Sportfive imetoa haki zote kwa Azam TV kuonyesha mechi zote za Yanga za Kombe la Shirikisho Afrika zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Azam wataonyesha mchezo wa kesho kati ya Yanga na TP Mazembe baada ya kupewa kibali cha kurekodi na kuonyesha mchezo huo na Sportfive au Lagardere Group ya Ufaransa.
 
Category: HABARI | Views: 319 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-27 | Comments (0)


 
MELI ya Mizigo ya Mv. Happy iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda  Zanzibar  imezama katika Bahari ya Hindi ikiwa imebeba mbao zaidi ya 1090 na magunia 450 ya viazi mviringo.
 
Hata hivyo,  mabaharia 12 ambao ni wafanyakazi katika meli ya mizigo  ya hiyo wamesalimika kufa maji  kwa vile meli hiyo  haikuzama yote  katika eneo la Kizingo  kisiwani Zanzibar.
 
Category: HABARI | Views: 388 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-27 | Comments (0)



Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo kuanzia jana. 
 
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema Rais amemteua Dk Charles Mlingwa ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha kujaza nafasi hiyo.
Category: HABARI | Views: 331 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-27 | Comments (0)


 

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameambiwa kuwa ni lazima alipe zaid ya dola nusu milioni pesa za umma, ambazo alitumia kukarabati nyumba yake.

Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imetaka wizara ya fedha, kutambua ikiwa ni kiaisi gasi Rais Zuma anasathili kurejesha kufutia uamuzi wa mapema mwaka huu kuwa alikuwa amekiuka katiba

Category: HABARI | Views: 278 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-27 | Comments (0)

Urusi inasema kuwa Rais Erdogan wa Uturuki ameomba msamaha kwa hatua ya taifa lake, kuidungua ndege ya kivita ya Urusi karibu na mpaka na Syria mwaka jana.

Katika ujumbe ulioandikwa ndani ya barua hadi Kremlin kwa Rais Putin, Bwana Erdogan alielezea masikitiko yake makubwa kwa kile kilichofanyika, huku akisema anataka kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Category: HABARI | Views: 304 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-27 | Comments (0)


 

BBC imebaini kuwa wanajeshi wa AMISON wanapigana vita na kundi la al shabab nchini Somalia hawajalipwa marupuru yao kwa miezi sita.

Kikosi hicho cha AMISOM kinafadhiliwa na Muungano wa Ulaya.

Taarifa za EU ziliiambia BBC kuwa malipo hayo ya miezi sita, yamezuiwa kutokana na matatizo ya kiuhasibu.

Category: HABARI | Views: 300 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-27 | Comments (0)