Home » 2016 August 17 » Vijana marufuku maandamano Morogoro
7:51 AM Vijana marufuku maandamano Morogoro |
Follow @NNurfire ![]() MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe, amewatahadharisha vijana wakiwemo wafanyabiashara wadogo kutokubali kushawishiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ili washiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu. Hivyo amewataka vijana hao watumie fursa ya amani na utulivu uliopo, kujituma kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kwa njia ya vikundi au mmoja mmoja kwa ajili ya maendeleo yao ya kiuchumi na kukuza pato la taifa. Mkuu wa Mkoa alisema hayo katika mkutano wa Umoja wa Viongozi wa Dini wa kuliombea amani taifa, uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wa madhehebu mbalimbali. Dk Kebwe alisema amani ya taifa ni tunu ambayo imeachwa na waasisi wa taifa akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliweka misingi mizuri. Alisema misingi iliyowekwa ya amani haipaswi kuharibiwa, badala yake inapaswa kutunzwa kwa nguvu zote bila kuanzisha chokochoko zitakazosababisha utulivu uliodumu kwa miaka mingi kutoweka. Aliwatahadharisha wanaojiandaa kuandamana, wasijaribu kufanya hivyo katika mkoa huo. Aliwaonya wafanyabiashara wa mkoa huo wasitumike kufanikisha malengo ya wanasiasa. Mkuu wa Mkoa, pia aliwaomba viongozi wa dini, kuisaidia serikali kufichua watu wanaohatarisha amani katika maeneo yao, kwa kuwa hatua hiyo itasaidia kulinda amani iliyopo na kuwezesha wananchi kuendelea kufanya shughuli zao za kujipatia kipato . |
|
|
| Total comments: 0 | |
