Home » 2016 » July » 08


Kutokana na hatari ya maambukizi ya ukimwi kukua katika shughuli za kutahiri teknolojia sasa imechukua nafasi kwaajili ya kupndoa hatari hiyo. Inakadiriwa kuwakiwango cha maambukizi ya ukimwi kimekuwa kikiongezeka katka tukio hilo huku ikisemekana imekuwa ikifanyika bila kukidhi taratibu. Shirika moja nchini Kenya limegundua kifaa kinachoweza kufanya kazi hiyo bila kuhitaji upasuaji wala kushonwa kwa aina yoyote ile. Tazama kwenye video zaidi kuhusiana na kifaa hicho. 
Category: VIDEOS | Views: 394 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)



Huku taarifa za mchezaji Paulo Pogba zikiwa zinazidi kushika nafasi kwenye vyombo vingi vya habari duniani kuhusu kujiunga na klabj ya Manchester united, kuna taarifa mpya kuhusu mchezaji huyo
Category: USAJIRI | Views: 477 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)




Manchester united imeambiwa isahau ndoto ya kumsajili mchezaji Hirving Lozino ambaye ameambiwa na klabu yake afute suala la kwenda Manchester united na hivyo anatakiwa ajikite kwenye klabu yake ya Pachuca. 
Category: USAJIRI | Views: 335 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)



Klabj ya Leicester city ya nchini Uingereza ambao pia ni mabingwa wa ligi kuu Uingereza wametakiwa kutoa kiasi cha £20 milioni ili kuweza kumsajili mchezaji Luan kutoka nchini Brazil. 
Category: USAJIRI | Views: 359 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)


Luol Deng amejiunga na timu ya mpira wa kikapu ya Marekani Los Angeles Lakers kwa thamani ya $72 milioni. Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Sudani pia amewahi kuiwakilisha Uingereza katika michuano ya Olympics iliyofanyika jijini London mwaka 2012.
Category: USAJIRI | Views: 359 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)



Huku ikiwa tayari imehusishwa sana na taarifa za kumsajili kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba klabu ya Manchester united ina taarifa mya kuhusu Blaise Matuid. 
 Kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa la L'Equipe limeripoti asubuhi hii kuwa klabu ya Ufaransa ya PSG ambayo ndiyo anayoitumikia Blaise Matuid imeipa ruhusa klabu ya Manchester united kufanya mazungumzo binafsi na mchezaji huyo ili kufikia makubaliano yatakayowezesha kufanikisha usajili wa mchezaji huyo kwenda Manchester united. 
Category: USAJIRI | Views: 382 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)



Wakala wa mchezaji wa timu ya soka ya Juventus na timu ya taifa ya Italia Leonardo Bonucci ametua nchini Uingereza. Taarifa zinasema kuwa wakala huyo ametua nchini humu ili kufanya mazungumzo na klabu ya Manchester city ambayo ipo kwenye harakati za kuhakikisha inamnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.
Category: USAJIRI | Views: 322 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)



Nchini Marekani leo polisi 11 wameshambjliwa kwa risasi na polisi 4 kati yao kuuawa baada ya washambuliaji kuwafyatulia risasi polisi hao katika tukio linaloonekana kuwa ni la kulipiza kisasi baada ya polisi mmoja nchini humo kumwua kijana wa kiafrika. 
Category: VIDEOS | Views: 342 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)


Kampuni inayojishughulisha na kutengeza programu maalum za kuzuia virus kwenye simu na kompyuta ya AVAST iko mbioni kuinunua kampuni nyingine ambayo pia inajihusisha na kutoa huduma hiyo hiyo kwa kiasi cha bilioni $1.3.
Category: HABARI | Views: 424 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali itahakikisha upungufu uliojitokeza katika mahakama mbalimbali nchini hautokei katika mahakama ya mafisadi yanayotarajia kuanza kazi hivi karibuni. Alisema upungufu kama vile ucheleweshaji wa upelelezi na kesi kuahirishwa mara kwa mara ndiyo sababu iliyofanya Rais John Magufuli kuunda mahakama hiyo.
Category: HABARI | Views: 342 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)


MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imewakumbusha wananchi kutoendelea kuwa na simu zilizozimwa majumbani mwao, na badala yake wazipeleke kwa watoa huduma au mamlaka hiyo ili ziharibiwe. Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba aliyesema si vyema wananchi kuendelea kuwa na simu zilizozimwa kwani zina kemikali zenye madhara.
Category: HABARI | Views: 282 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)


Mkakati wa Chadema kwenda kuzuia mkutano mkuu wa CCM utakaofanyika mkoani Dodoma, umemfikisha polisi Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa (Bavicha), Patric Ole Sosopi kwa madai ya kutoa lugha chafu inayotishia uvunjifu wa amani nchini.
Category: HABARI | Views: 336 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)


Rais John Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara. Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
Category: HABARI | Views: 351 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)

MSEMAJI wa Yanga, Jerry Muro amefungiwa kujihusisha na soka kwa mwaka mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Sh 3 Milioni. Taarifa iliyopatikana jioni hii ilieleza kuwa Kamati ya Maadili ya TFF iliyokutana jijini Dar es Salaam chini ya mwenyekiti wake, Wilson Ogunde imefikia hatua hiyo baada ya kuyachambua makosa matatu yaliyokuwa yakimkabili.
Category: MICHEZO | Views: 316 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)



Kocha mpya wa klabu ya soka ya Manchester united ya nchini Uingereza rasmi ameanza kazi baada ya kujiunga na klabu hiyo hivi karibuni.Ifuatayo ni orodha nzima ya benchi la ufundi la timu hiyo
Category: MICHEZO | Views: 405 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-08 | Comments (0)