Home » HABARI
« 1 2 ... 23 24 25 26 27 ... 32 33 »



Hatimaye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson ametoa maamuzi kuhusu hoja ya wabunge kulipwa posho au kutolipwa wanapoingia Bungeni na baadae kutoka nje kwa shughuli zisizo za Kibunge.
Akisoma muongozo wake muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge jioni hii baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango kusoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, Dk. Tulia alisema kuwa wabunge wanaofanya vitendo hivyo hawatalipwa posho.
 
Category: HABARI | Views: 279 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-09 | Comments (0)



Serikali ya Nigeria imetangaza mpango wa kutoa ajira kwa vijana zaidi ya nusu milioni ambao wamemaliza chuo kikuu lakini hawana ajira, hatua hii ni mojawapo ya jitihada za serikali za kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Mpango huo ni sehemu ya uwekezaji katika jamii ulioahidiwa na rais Muhammadu Buhari wakati wa kampeni yake ya kugombea urais.
Category: HABARI | Views: 310 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-09 | Comments (0)



Waziri wa fedha nchini Uganda Matia Kasaija amesema kuwa maafisa huenda wakafutwa kazi iwapo watapatikana wamefanya safari zisizo na maana kwa kutumia fedha za serikali.

Tangazo hilo ni miongoni mwa hatua za kubana matumizi ya fedha za serikali ili kusaidia kufadhili miradi mingine

 
Category: HABARI | Views: 301 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-09 | Comments (0)



Watoto sita wamekufa maji bila kutarajiwa katika sherehe za kubatizwa kwao katika mto nchini Zimbabwe.Watoto watatu walinusurika kufa maji ya mto huo ambao maji yake niya baridi;watoto hao walionekana wakitetemeka kutokana na baridi wakati miili ya wenzao waliokufa maji ikiopolewa majini.
Category: HABARI | Views: 340 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-09 | Comments (0)

Viongozi na makada wa Chadema waliokuwa wakisafiri kutoka Kahama kuelekea jijini Mwanza jana wamejikuta wakishindwa kuingia kwenye ofisi za chama hicho mjini Shinyanga kutia saini kitabu cha wageni baada ya Jeshi la Polisi kuzuia shughuli yoyote ya chama hicho mjini humo.
Category: HABARI | Views: 262 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-09 | Comments (0)

Wanamuziki kutoka Nigeria Tiwa Savage na Don jazzy wamekutana na mwanamuziki maarufu duniani Jay -Z.Wasanii hao wamekutana na mkali huyo kwenye makao makuu ya ofisi za Rock nation.
Wasnii hao wapo mbioni kukamilisha dili ya Savage kuweza kusaini mkataba na lebo hiyo ya Jay-Z

Category: HABARI | Views: 304 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-08 | Comments (0)

Waziri Mkuu wa Uingereza na mpinzani wake anayetaka Uingereza kujitenga na Muungano wa ulaya, Nigel Farage, wameulizwa maswala makali kuhusu athari za Uingereza kujiondoa kwenye muungano huo wakati wa mdahalo wa Runinga.

Category: HABARI | Views: 279 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-08 | Comments (0)

Bi Hillary Clinton amesema ameshinda uteuzi wa urais wa chama cha Democratic, kufuatia ushindi wake katika uteuzi wa mashinani katika jimbo ya New Jersey na pia uungwaji mkono unaotarajiwa kutoka kwa wajumbe maalum.

Category: HABARI | Views: 313 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-08 | Comments (0)



Serikali ya Kenya imepiga marufuku maandamano ya aina yoyote nchini humo, kufuatia vifo vya watu kadhaa, baada ya ghasia kukumba taifa hilo la Afrika Mashariki, yaliyoandaliwa na muungano wa upinzani CORD.
Hayo yamesemwa hivi punde na waziri wa usalama wa ndani nchini humo, Bwana Joseph Nkaissery, katika kikao na wanahabari.
Category: HABARI | Views: 320 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-08 | Comments (0)



Hatua hiyo ya aina yake kuonekana katika nchi nyingi barani Afrika, imechukuliwa kwa nia ya kutimiza kwa vitendo lengo la Serikali ya Awamu ya Tano la kubana matumizi ili kiasi kitakachookolewa kielekezwe katika miradi ya maendeleo inayowagusa wananchi wa kawaida.
Category: HABARI | Views: 295 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-08 | Comments (0)