Home » HABARI
« 1 2 ... 21 22 23 24 25 ... 32 33 »
Waziri wa michezo wa urusi Vitaly Mutko, anasema kuwa anaelewa kuwa huenda taifa lake likapigwa faini na shirikisho la soka la bara ulaya kutokana na tabia isiyofaa ya mashabiki wa timu ya taifa hilo.

UEFA, imeanza uchunguzi wa machafuko makali yaliyotokea baada ya mechi ya dimba la EURO kati ya Urusi na Uingereza katika mji wa Marseille nchini Ufaransa.
Category: HABARI | Views: 316 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-12 | Comments (0)


Ripoti kutoka Iraq zinasema vikosi vya serikali vimeshambulia wapiganaji wa Islamic state kusini mwa mji wa Mosul.

Taairfa za kijeshiznasema kuwa vikosi vimekuwa vikisogelea mji huo kwa kutumia vifaru na magari ya kivita, wakiungwa mkono na vikosi vya angani vinavyoongozwa na marekani.

Mashambulizi hayo yanaonekana kulenga ngome muhimu ya Islamic state kaskazini mwa taifa hilo.
Category: HABARI | Views: 352 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-12 | Comments (0)


Polisi katika mji wa Orlando nchini marekani wanasema kuwa watu wengi wamepigwa risasi katika baa moja ya usiku.

Inaarifiwa kuwa takriban watu 20 wamejeruhiwa katika baa hiyo kwa jina Pulse, na kuwa mwanamme aliyejihami kwa bunduki aliwateka watu wengine.
 
Category: HABARI | Views: 280 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-12 | Comments (0)



KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwafutia posho wabunge wote wanaofika kwenye vikao vya Bunge hilo na kukaa kimya bila kuchangia jambo lolote hata kwa maandishi kwa maelezo kuwa hawafanyi kazi.
Category: HABARI | Views: 297 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-12 | Comments (0)




WANAFUNZI wa Darasa la tano mpaka la saba katika shule ya msingi Mbande katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wameunda makundi yanayolalamikiwa kuwa ndio chanzo cha wanafunzi kutosoma. Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema ameamuru wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Category: HABARI | Views: 293 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-12 | Comments (0)



TASISI ya Benjamin Mkapa itaikabidhi Serikali nyumba 258 za madaktari, wauguzi na wafamasia katika mikoa mbalimbali hadi ifikapo Julai 30, mwaka huu. Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Dk Ellen Mkondya- Senkoro, alisema lengo la taasisi hiyo kujenga nyumba hizo ni kuisaidia serikali kutatua matatizo mbalimbali yaliyopo katika sekta ya afya, mfano ukosefu wa nyumba za watumishi wa afya.
Category: HABARI | Views: 261 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-12 | Comments (0)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri huku akimteua Mbunge wa Buchosha Dk. Charles Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Category: HABARI | Views: 325 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)



Ifuatayo ni miji 16 yenye mifumo ya usafiri ambayo ni hatari zaidi kwa wanawake. 
Category: HABARI | Views: 290 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)



Watu sita wamefariki Dunia na wengine nane wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Hiace lililokuwa likitokea Mjini Same likielekea Njoro Wilayani Same, ambapo liligongana na gari ya mizigo aina ya Fuso muda mfupi baada ya kuondoka katika Kituo cha abiria cha Same Mjini.
Category: HABARI | Views: 316 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)

MLALAMIKIWA wa kwanza katika kesi ya uchaguzi Jimbo la Longido mkoa wa Arusha, Mbunge wa Longido, Onesmo ole Nangole (Chadema), ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuwa anajua kusoma na kuandika Kiswahili, lakini hajui kusoma na kuandika Kiingereza.
Category: HABARI | Views: 324 | Added by: nurdidy | Date: 2016-06-11 | Comments (0)