Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe, Charles Nakembetwa alimtaja mwanasheria huyo kuwa ni Frednand Nsakuzi na Julius Hasani ambaye ni mlinzi wa ofisi ya taasisi hiyo.
Category: HABARI |
Views: 362 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-07-02
|
|
WAKATI Mahakama Maalumu ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi ikitarajiwa kuanza wakati wowote, majengo ya mahakama hiyo yanatarajiwa kukabidhiwa keshokutwa.
Category: HABARI |
Views: 376 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-07-02
|
|
Serikali ya nhini Kenya imetangaza kua siku ya Ed el Fitri, siku ambayo waumini wa kiislamu wanategemea kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni siku ya mapumziko kitaifa. Kwa mjjibu wa serikali ya Kenya siku iliyotangazwa ni tarehe 7 julai.
Category: HABARI |
Views: 268 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-07-02
|
|
WATU 11 wamekufa papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea sehemu moja, zikihusisha basi la abiria, lililopamia malori mawili ya mizigo yaliyogongana uso kwa uso na kuungua moto eneo la Dakawa – Veta, wilayani Kilosa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema mjini hapa jana kuwa ajali ya kwanza, malori mawili ya mizigo yaligongana uso kwa uso juzi saa 12 jioni na kuwaka moto.
Category: HABARI |
Views: 283 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-07-02
|
|
UJENZI wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa cha standard gauge, unatarajiwa kuanza kwa vipande vipande na wakandarasi tofauti; mmoja kutoka Dar es Salaam kwenda Kigali na mwingine kutoka Kigali kwenda Dar es Salaam, ili kuharakisha ukamilishaji wake.
Category: HABARI |
Views: 328 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-07-02
|
|

Leo ndiyo mwanzo wa utekelezaji wa Sheria Fedha (Finance Act, 2016) iliyopitishwa katika Bajeti ya 2016/17 ambapo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) itatozwa katika huduma za mitandao ya simu, benki na taasisi za fedha.
Akisoma hotuba ya bajeti bungeni hivi karibuni, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango pamoja na mambo mengine, alipendekeza kuongeza kodi hiyo katika huduma za kibenki zinazotozwa na benki hizo ili kupanua wigo wa kodi isipokuwa riba kwenye mikopo.
Category: HABARI |
Views: 294 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-07-01
|
|

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) hatimaye wametaja mfanyabiashara ambaye alibainishwa na Rais John Magufuli katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Ikulu Dar es Salaam juzi.
Category: HABARI |
Views: 284 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-07-01
|
|
Baada tu ya juzi kutolewa taarifa kutoka TRA kuhusu ongezeko la kodi ya VAT kwa asilimia 18% mabenki nchini yalianza kutuma ujumbe wa simu kwa wateja wao kuwajulisha kuhusu ongezeko hilo huku yakionyesha mzigo huo kubebwa na wananchi. Leo mamlaka husika inayosimamia kodi hiyo yaani TRA imetoa ufafanuzi kuhusu hilo kama inavyoonyesha hapo juu.
Category: HABARI |
Views: 354 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-07-01
|
|

Korea Kusini, Marekani na Japan zimefanya zoezi la ushirikiano la kukabiliana na makombora katika maji ya jimbo la Hawaii.
Hatua hiyo inajiri kufuatia msururu wa majiribio ya makombora ya masafa mafupi katika miezi ya hivi karibuni inayofanywa na Korea kaskazini.
Category: HABARI |
Views: 290 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-29
|
|
Uingereza imezuia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ulaya ambapo itakuwa mara ya kwanza kufanyiwa hivyo kwa miaka 40.
Waziri Mkuu, David Cameron, hatakuwa mezani wakati viongozi wengine 27 wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Ulaya watakuwa wakihudhuria mkutano usio rasmi juu ya hatma ya muungano huo baada ya kuondoka kwa Uingereza.
Category: HABARI |
Views: 315 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-29
|
|
|