Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Lwema ametishia kumburuza mahakamani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Godfrey Sanga kwa madai ya kuendelea kutoza ushuru wa mazao baada ya kufutwa na Serikali mwaka 2002.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe ameridhia kufutwa kwa bodi za wadhamini na taasisi mbalimbali zisizokuwa za kiserikali 680 ambazo haziko kisheria. Pamoja na hayo kairuhusu Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuzisajili upya wadhamini wa asasi, na taasisi mbalimbali.
Kituo cha televisheni cha Clouds kimetakiwa kuomba radhi kwa siku tano kupitia taarifa zake za habari kutokana na maudhui ya kipindi cha Take One kilichomuonyesha mwanaume anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Kampuni inayojishughulisha na kutengeza programu maalum za kuzuia virus kwenye simu na kompyuta ya AVAST iko mbioni kuinunua kampuni nyingine ambayo pia inajihusisha na kutoa huduma hiyo hiyo kwa kiasi cha bilioni $1.3.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali itahakikisha upungufu uliojitokeza katika mahakama mbalimbali nchini hautokei katika mahakama ya mafisadi yanayotarajia kuanza kazi hivi karibuni. Alisema upungufu kama vile ucheleweshaji wa upelelezi na kesi kuahirishwa mara kwa mara ndiyo sababu iliyofanya Rais John Magufuli kuunda mahakama hiyo.
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imewakumbusha wananchi kutoendelea kuwa na simu zilizozimwa majumbani mwao, na badala yake wazipeleke kwa watoa huduma au mamlaka hiyo ili ziharibiwe. Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba aliyesema si vyema wananchi kuendelea kuwa na simu zilizozimwa kwani zina kemikali zenye madhara.
Mkakati wa Chadema kwenda kuzuia mkutano mkuu wa CCM utakaofanyika mkoani Dodoma, umemfikisha polisi Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa (Bavicha), Patric Ole Sosopi kwa madai ya kutoa lugha chafu inayotishia uvunjifu wa amani nchini.
Rais John Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara. Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
MAZIKO ya Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilindi, mkoani Tanga, Beatrice Shelukindo (CCM), yanatarajiwa kufanyika leo nyumbani kwa wazazi wake, Kata ya Olorieni jijini hapa.
Kaka wa marehemu, Enock Madinila alisema maziko hayo yalikuwa yafanyike kesho katika kata hiyo, lakini yamerudishwa nyuma kwa siku moja kutokana na sababu zilizoelezwa na familia kuwa wamezingatia mambo kadhaa.