 Wabunge wanatarajiwa kukatwa asilimia 30 ya kiinua mgongo chao ambacho kimeelezwa kuwa ni Sh200 milioni.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwenye Kamati ya Bajeti iliyopitia muswada huo, zimeeleza kuwa asilimia hiyo inatokana na marekebisho yaliyofanywa na kupitishwa na wabunge wenyewe kwenye Sheria ya Mapato ya 2010.
Category: HABARI |
Views: 280 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-20
|
|
Wakati Kamati ya Haki, Maadili na Madara ya Bunge imepokea mashtaka dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, mbunge mwingine wa upinzani ameamua kumshtaki kiongozi huyo kwenye Kamati ya Kanuni ya Bunge.
Category: HABARI |
Views: 304 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-20
|
|
Kampuni ya Microsoft imekuwa ya hivi karibuni kujiunga na biashara ya kuuza bangi katika majimbo ya nchini Marekani ambako inaruhusiwa kwa mujibu wa sheria za majimbo hayo.
Kampuni hiyo imeungana na kampuni nyingine "Kind Financial - inayotengeneza programu za kusaidia wadhibiti kufuatilia uzalishaji na mauzo ya bangi.
Majimbo kadhaa nchini Marekani yameruhusu uuzaji wa bangi kwa matumizi ya kimatibabu na kujistarehesha, japo imeharamishwa chini ya sheria kuu za nchi hiyo.
Category: HABARI |
Views: 366 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-18
|
|

Timu ya taifa ya Italia imefika hatua ya muondoano katika michuano ya ubingwa wa Ulaya baada ya kujipatia ushindi dhidi ya Sweden.
Ushindi wa Italia ulitokana na bao la pekee la mechi hiyo, lililofungwa na Eder dakika za mwishomwisho.
Ishara zilionesha kana kwamba mechi hiyo ingemalizika sare tasa hadi pale Eder alipokimbia na kufikia mpira kutoka kwa Simone Zaza nje kidogo ya eneo la hatari dakika ya 88.
Category: HABARI |
Views: 287 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-18
|
|
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kushirikiana na viongozi wa Mkoa kuhakikisha kuanzia leo hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara katika maeneo ya ‘mataa’
Category: HABARI |
Views: 304 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-18
|
|
IDARA ya Uhamiaji iko katika mchakato wa kuanzisha mahakama ya kijeshi ili kuwaadhibu maofisa wake wanaokiuka taratibu kama ilivyo kwa majeshi mengine nchini.
Hayo yalisemwa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusufu Masauni, wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge.
Category: HABARI |
Views: 335 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-18
|
|
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo, amewataka wabunge kuacha kuwapelekea viongozi ‘vimemo’ vya kuwaombea msamaha watumishi wasio na maadili wa hospitali mbalimbali nchini watakapokuwa wanatumbuliwa.
Category: HABARI |
Views: 316 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-18
|
|
TAMASHA la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, linaloandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, limetoa tuzo ya pekee kwa mwanzilishi wa Vikundi vya Benki za Kijamii (Vicoba), anayejulikana kwa jina la George Swevetta kwa mchango wake wa kukuza na kuimarisha uchumi kwa watu nchini.
Category: HABARI |
Views: 354 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-18
|
|
MTOTO mwenye ulemavu wa ngozi (albino) mwenye umri wa miaka mitatu, mkazi wa wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu hivi karibuni amenusurika kuuawa kwa kukatwa mapanga, baada ya bibi yake kudaiwa kumuuza kwa wauaji hao ili waweze kuchukua sehemu ya viungo vyake.
Category: HABARI |
Views: 303 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-18
|
|
|
Akizungumza baada ya mtendaji huyo kuhamishwa, mmoja wa wakazi hao, Ernest Bunyutule amesema jana kuwa: “Mtendaji huyu ameonyesha uwezo mkubwa kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kutatua kero za wananchi. Hatupo tayari kumpokea mtendaji mwingine.”
Category: HABARI |
Views: 286 |
Added by: nurdidy |
Date: 2016-06-18
|
|
|