Home » HABARI
« 1 2 ... 12 13 14 15 16 ... 32 33 »


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime mkoani Mara kimewaonya vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaodai kuwa watakwenda Dodoma kufanya vurugu katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM mwishoni mwa wiki hii, wasithubutu kufanya hivyo.
Category: HABARI | Views: 268 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-18 | Comments (0)



SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la JhPiego limekabidhi jengo jipya la wadi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera lenye thamani ya Sh mil 136.5, linalotegemewa kusaidia kupunguza msongamano katika wadi ya wazazi, pamoja na vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
Category: HABARI | Views: 353 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-18 | Comments (0)



MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu amefunguka kuhusu mambo juu ya utendaji wa jeshi hilo na kueleza kuwa wakati wowote litamburuza mahakamani Katibu Mkuu wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuhamasisha uchochezi visiwani Zanzibar.
Category: HABARI | Views: 329 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-18 | Comments (0)




​Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).
Category: HABARI | Views: 323 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-18 | Comments (0)



Marekani imeitaka Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.
Category: HABARI | Views: 306 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-17 | Comments (0)




Maelfu ya raia wa nchi ya Venezuela wamevuka mpaka na kuingia maeneo ya karibu ya nchi ya Colombia kwaajili ya kununua vyakula na madawa baada ya mpaka baina ya nchi hiyo kufunguliwa kufuatiwa kuwa umefungwa kwa karibu mwaka mzima. 
Category: HABARI | Views: 291 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-17 | Comments (0)


Waziri Mkuu wa Uturuki, Binali Yildirim, ameelezea jaribio la mapinduzi la jana usiku, kuwa doa jeusi katika demokrasi ya Uturuki.
Na kaimu mkuu wa jeshi la Uturuki, ametangaza kwenye televisheni, kwamba jaribio la mapinduzi limeshindwa. Jenerali Umit Dundar alisema, wapanga njama 104 wameuwawa.
 
Category: HABARI | Views: 296 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-17 | Comments (0)



Baada ya uvumi na taarifa kuenea kuwa wizara ya afya ina mpango wa kupunguza mishahara ya madaktari hatimaye waziri wa fedha Ummy Mwalimu wametoa ufafanuzi kupitia akaunti zao za twitter na haya ndiyo maneno yao. 
Category: HABARI | Views: 383 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-10 | Comments (0)



WAUMINI zaidi ya 300 kutoka mikoa mbalimbali nchini waliokuwa wameweka kambi kwa ajili ya kushiriki kongamano la Kanisa la Sauti ya Uponyaji la Nabii Joshua, eneo la Kihonda- Veta, Manispaa ya Morogoro wamelazimika kurejea makwao kutokana na kongamano hilo kusitishwa, baada ya baadhi yao kuugua ugonjwa wa kipindupundu na kulazwa kambi maalumu ya Kituo cha Afya cha Sabasaba cha mjini Morogoro.
Category: HABARI | Views: 328 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-09 | Comments (0)



HUZUNI imetanda katika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, baada ya ajali ya moto wa kibatari kuteketeza watoto wanne wa mama mmoja, waliokuwa wamefungiwa chumbani na dada anayewalea.
Category: HABARI | Views: 279 | Added by: nurdidy | Date: 2016-07-09 | Comments (0)